Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Mayala Towo, alimtaja dereva
anayeshikiliwa kuwa ni Saidi Juma (26) mkazi wa Dodoma ambaye inadaiwa
siku ya tukio alikuwa anaendesha basi aina ya Nissan Civilian lenye
namba za usajili T.360 DAY huku akicheza muziki.
Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 4, mwaka huu, saa 11: 00
jioni katika Mji Mdogo wa Itigi wilayani Manyoni wakati mtuhumiwa akiwa
na wenzake watatu, alipoendesha gari hilo kwa mwendo wa hatari kwa
kucheza muziki huku akiachiana usukani na wenzake hao wakati gari hilo
likiwa kwenye mwendo.
Kamanda Towo aliwataja watuhumiwa wengine ambapo pia wanashikiliwa na
Polisi kuwa ni Joseph Ramadhan (27), Ezekiel Joseph (24) na Sebastian
Godfrey (23) wote wakazi wa Majengo, Itigi.
Social Plugin