Mbunge Godbless Lema amerejeshwa tena rumande leo baada ya rufaa yake ya kupinga kunyimwa dhamana kushindikana kusikilizwa kama ilivyokuwa imepangwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo.
Rufaa hiyo ya Lema iliyokuwa umepangwa kusikilizwa leo imeshindikana baada ya upande wa Jamhuri kukata rufaa kupinga kuongezwa muda wa kuwasilisha notisi ya rufaa.
Mawakili wa Lema waliomba kuongezewa muda wa kuwasilisha notisi ya kukata rufaa kupinga kunyimwa dhamana baada ya kushindwa kufanya hivyo katika muda uliokuwa umepangwa awali.
Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya rufaa hizo Salma Magimbi amesema kuwa mara baada ya upande wa jamhuri kuleta rufaa kwa njia ya maandishi upande wa mshtakiwa Lema wataijibu tarehe 30 Disemba 2016 ambapo tarehe 2 Januari watakutana pande zote kwa ajili ya kufanya majumuisho na maamuzi ya rufaa hiyo yatatolewa tarehe 4 Januari 2017.
Mbunge Godbless Lema ambaye alikamatwa Novemba 2 mwaka huu mjini Dodoma amerejeshwa rumande katika gereza la Kisongo jijini Arusha.
Social Plugin