Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara amejitokeza kwa mara ya kwanza kumuombea msamaha mtani wake Jerry Muro ili kuifufua upya hamasa na kuongeza ushindani katika ulimwengu wa soka la Bongo.
Jerry Muro ambaye ni Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga amefungiwa na TFF kwa muda wa mwaka mmoja kutojihusisha na soka kutokana na matumizi mabaya ya kauli zake kupitia vyombo vya habari mwezi Julai mwaka huu.
Manara katika ujumbe aliouweka kwenye mtandao wake wa Instagram akiuelekeza kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi, amesema katika kuadhimisha sikukuu ya Krismasi anaona ni wakati muafaka sasa kwa Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia Jerry kwa kuwa amekwishatumikia takriban nusu ya kifungo chake na kwamba soka la Bongo linamuhitaji sana kwa sasa.
"Nimekaa nimetafakari sana,nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, ninafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake, ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla. "Ameandika Manara
Manara pia hakusita kukumbushia jinsi ambavyo Jerry Muro amewahi kumtolea hata yeye mwenye lugha za kuudhi "
Nnafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi bnafsi, lakini yale yashapita na binafasi amenihakikishia kutorudia tena, na nnaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wanasimba".
manara amemaliza kwa kusema kuwa soka la Tanzania linammis sana Jerry Muro na kuomuomba Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia kwa kuwa Jerry bado alikuwa hajawa na uzoefu wa kutosha katika siasa za mpira.
Kwa upande wake Jerry Muro amefurahi na kushukuru kuona mtani wake Haji Manara anamkumbuka na kutumia fursa hiyo kuomba msamaha kwa shirikisho la soka Tanzania ili aendeleze hamasa ya soka aliyokuwa ameiweka nchini yeye na Haji Manara.
Social Plugin