Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 03 Desemba, 2016 amefanya uteuzi wa Mabalozi 15 ili kujaza nafasi zilizo wazi katika Balozi za Tanzania zilizopo katika nchi mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mabalozi hao wameteuliwa kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika vituo vifuatavyo;
- Beijing - China
- Paris - Ufaransa
- Brussels - Makao Makuu ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya
- Muscat - Oman
- Rome - Italy
- New Delhi - India
- Pretoria - Afrika ya Kusini
- Nairobi - Kenya
- Brasilia - Brazil
- Maputo - Msumbiji
- Kinshasa - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
- Kampala - Uganda
- Abuja - Nigeria
- Moroni - Comoro
- Geneva - Umoja wa Mataifa
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Mabalozi 6 kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Balozi mpya 6 ambazo zitafunguliwa hivi karibuni katika nchi za Algeria, Israel, Korea ya Kusini, Sudan, Qatar na Uturuki.
Orodha kamili ya Mabalozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
- Balozi Mbelwa Brighton Kairuki
- Balozi Samuel W. Shelukindo
- Balozi Joseph E. Sokoine
- Balozi Silima K. Haji
- Balozi Abdallah Kilima
- Balozi Baraka Luvanda
- Balozi Dkt. James Alex Msekela
- Balozi Mteule Sylvester Mwakinyuke Ambokile
- Balozi Mteule Pindi Chana
- Balozi Mteule Dkt. Emmanuel J. Nchimbi
- Balozi Mteule Rajab Omari Luhwavi
- Balozi Mteule Lut. Jenerali (Mstaafu) Paul Ignace Mella
- Balozi Mteule Grace Mgovano
- Balozi Mteule Mohamed Said Bakari
- Balozi Mteule Job Masima
- Balozi Mteule Omar Yusuf Mzee
- Balozi Mteule Matilda S. Masuka
- Balozi Mteule Fatma M. Rajab
- Balozi Mteule Sylvester M. Mabumba
- Balozi Mteule Prof. Elizabeth Kiondo
- Balozi Mteule George Madafa (Uteuzi wake ulishatangazwa)
Vituo vya kazi vya mabalozi hawa 21 vitatangazwa baadaye.
Mabalozi wote waliobaki katika vituo ambavyo si kati ya vituo hivi 15 vilivyotajwa wataendelea na nafasi zao za uwakilishi wa Tanzania katika vituo walivyopo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemhamisha Balozi Modest Jonathan Mero kutoka kituo chake cha sasa cha Geneva, kwenda Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (New York) ambako atakuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Mhe. Balozi Modest Jonathan Mero anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Tuvako M. Manongi ambaye atastaafu ifikapo tarehe 06 Desemba, 2016.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi Grace A. Martin kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Itifaki (Chief of Protocal) – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kuanzia leo tarehe 03 Desemba, 2016.
Kabla ya uteuzi huo Bibi Grace A. Martin alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Balozi Peter Kallaghe kuwa Afisa Mwandamizi Mwelekezi – Mambo ya Nje katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College)
Kabla ya uteuzi huo, Balozi Peter Kallaghe alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza hadi mwanzoni mwa mwaka huu 2016.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Desemba, 2016
Social Plugin