Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga ambaye sasa yuko Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Khamis Mgeja akiwa na Mbunge Mstaafu wa jimbo la Nzega Lucas Selelii (kulia) juzi alipokwenda kumpa pole Mbunge huyo aliyefiwa na mke wake hivi karibuni maeneo ya Uzunguni mjini Nzega mkoani Tabora.
Mbunge huyo mstaafu Lucas Selelii kupitia CCM alitumia nafasi hiyo kumshawishi Mgeja arudi CCM ili washirikiane kujenga chama.
Hata hivyo Mgeja alisema pamoja na kumheshimu mbunge huyo mstaafu kama kaka na rafiki yake, bado haoni sababu ya kurudi CCM akidai sababu zilizomfanya ahame CCM ziko pale pale na hana sababu zingine zinazoweza kumfanya arudi CCM.

Mgeja akiwa nyumbani kwa mbunge mstaafu wa jimbo la Nzega Lucas Selelii
Social Plugin