Paul Kayanda akipanda kwenye gari la polisi leo Ijumaa Desemba 30,2016 |
Mwandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Paul Kayanda amefikishwa mahakamani kwa agizo la Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu kwa madai kuwa mwandishi huyo wa habari anamchafua kwa njia ya email.
Mwandishi huyo anadaiwa kuandika habari kuhusu mkuu huyo wa wilaya kuibiwa laptop mbili nyumbani kwake kisha kuwaweka ndani/polisi kwa muda wa siku saba watu watatu akiwemo kijana anayeishi naye nyumbani bila kuwafikisha mahakamani.
Mwandishi huyo alikamatwa leo asubuhi kisha kufikishwa katika mahakama ya wilaya kisha kurudishwa tena polisi kutokana na kukosekana kutokuwepo kwa shtaka lolote lililofunguliwa kutoka polisi kwenda mahakamani.
Hata hivyo baada ya kurudishwa polisi,alifikishwa katika wilaya ya Mwanzo wilayani humo na kusomewa mashtaka ya kumchafua mkuu huyo wa wilaya kisha kuachiwa kwa dhamana na kutakiwa kurudi mahakamani Januari 02,2017.
Mkuu huyo wa wilaya amesema mwandishi wa habari huyo amefikishwa mahakamani kutokana na kuandika habari za kumchafua kwa kusambaza habari kupitia email na kumtumia sms alizodaiwa siyo za maadili.
TAARIFA
KWA UMMA
Uongozi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
(SPC) umefuatilia kwa undani suala la mwandishi wa habari Paul Kayanda
kufikishwa mahakamani kwa agizo la mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu kwa
kile kinachotajwa kuwa ameandika habari za kumchafua baada ya mkuu huyo wa
wilaya kuibiwa laptop mbili nyumbani kwake.
Uongozi wa klabu umefanya mazungumzo na viongozi mbalimbali
wa serikali akiwemo mkuu huyo wa wilaya ya Kahama lakini pia na mwandishi Paul
Kayanda kuhusu suala hilo.
Kutokana na suala hilo kuwa na utata tumekubaliana kesho
Jumamosi Desemba 31,2016 saa tano asubuhi,uongozi wa klabu ya waandishi wa habari,waandishi
wa habari walioko wilayani Kahama na mkuu huyo wa wilaya tutakutana katika kikao cha pamoja kwa ajili
ya kuzungumzia suala hilo na kutafuta utatuzi wake hivyo yatakayojiri
tutawatarifu.
Imetolewa na
Kadama Malunde
Mwenyekiti SPC
Social Plugin