NAPE NNAUYE AWAOMBA RADHI VIONGOZI NA WAFUASI WA VYAMA VYA UPINZANI TANZANIA

Alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amewaomba radhi viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini kwa lolote ambalo aliwakwaza wakati akitekeleza majukumu yake katika nafasi hiyo.



Nape amewaangukia wapinzani pamoja na makundi mengine ya watanzania ikiwemo viongozi wenzake ndani ya chama leo wakati akikabidhi rasmi ofisi kwa kiongozi mpya anayechukua nafasi hiyo, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam, Humphrey Polepole katika ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho, Lumumba Jijini Dar es Salaam.


"Nawaomba msamaha viongozi wenzangu, wanachama, waandishi na hata wapinzani pale ambapo nimewaumiza katika kufanya kazi yangu, samahani sana. Nategemea ushirikiano niliopatiwa mimi na wanahabari utaendelea kwa ndugu yangu Humphrey Polepole, ni mtu mwenye weledi mpana" amesema Nape


Nape pia amekiri kuwa chama hicho kimemsaidia zaidi kwenye maisha yake kuliko yeye alivyokisaidia wakati akiitumikia nafasi hiyo.


"Nakiri mbele yenu kuwa chama kimenisaidia zaidi kuliko mimi nilivyokisaidia Chama, nashukuru Mungu kuwa nimemaliza kazi hii salama, nilipata wosia wa Mzee Kinana kuwa nishukuru nikimaliza salama"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post