Picha 40 : MFUMO WA JAZIA DAWA,VIFAA TIBA NA VITENDANISHI ‘PRIME VENDORS SYSTEM’ WAZINDULIWA SHINYANGA



Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na mradi wa Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na shirika serikali ya Uswizi leo Jumanne Desemba 13,2016 umezindua Mpango wa Mzabuni teule “Mfumo wa Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi”.

Mfumo wa Jazia dawa,vifaa tiba na vitendanishi kwa kutumia mzabuni Teule Mmoja ‘Prime Vendor’ ni moja ya mafanikio ya ushirikiano wa sekta binafsi na serikali ukiwa na lengo la kujazia upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya umma vya kutolea huduma za afya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,katibu tawala wa mkoa huo Albert Msovela aliyekuwa mgeni rasmi alisema lengo la mfumo huo ni kuziba pengo linalosababishwa na ukosefu wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya afya kutoka Bohari kuu ya dawa.

Alisema kutokana na bohari ya dawa ya serikali kutokidhi mahitaji kila halmashauri hununua dawa kutoka kwa wazabuni wanaowataka matokeo yake bei ya dawa inakuwa kubwa,mlolongo mrefu wa manunuzi na kukosekana kwa njia rahisi ya usimamizi wa mfumo wa ugavi na usambazaji.

"Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na mradi wa Tuimarishe Afya( HPSS Project) unaofadhiliwa na serikali ya Uswizi kupitia shirika lake la Maendeleo (SDC) umeamua kutafuta njia ya kuziba pengo linalosababishwa na ukosefu wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi kutoka bohari kuu ya dawa kwa kutumia mfumo wa manunuzi ya nje ya bohari kuu unaohusisha mzabuni mmojatu kwa mkoa mzima,ambaye sasa Bahari Pharmacy Limited",alieleza Msovela.

Naye mwakilishi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Siana Mapunjo alisema mkoa wa Shinyanga ni wa pili baada ya Mkoa wa Dodoma kuanza kutekeleza Mpango wa Mzabuni teule huku akisisitiza halmashauri kusimamia matumizi bora ya dawa na wazee kuendelea kupewa kipaumbele.


Uzinduzi huo umehudhuriwa na wakuu wa wilaya,Mkurugenzi wa Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS),mkurugenzi wa MSD,Mfamasia mkuu wa serikali,mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri,waganga wakuu wa halmashauri na wageni mbalimbali.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametusogezea picha 40 kutoka kwenye uzinduzi huo….Tazama Hapa Chini
Kwa kwanza kushoto ni Meneja wa mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga Dr. Harun Kasale,katikati ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli Kapologwe na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Desemba 13,2016 wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Mzabuni Teule “Prime Vendor System” yaani Mfumo Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi ambapo alisema mfumo huo utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika mkoa wa Shinyanga .Aliongeza kuwa bohari ya dawa ina uwezo wa kuhudumia wateja kwa asilimia 57 pekee katika mkoa wa Shinyanga.
Wa kwanza kulia ni kaimu mkurugenzi wa idara ya Ununuzi na Ugavi ofisi ya rais TAMISEMI Datus Matuma,katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya afya ofisi ya rais TAMISEMI Deogratius Maufi.Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Siana Mapunjo 
Wadau mbalimbali wa afya mkoani Shinyanga 
Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Mzabuni Teule “Prime Vendor System” yaani Mfumo Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi una lengo la kujazia dawa kwenye vituo vya serikali vya kutolea huduma za afya.
Kulia ni kaimu mkurugenzi wa idara ya Ununuzi na Ugavi ofisi ya rais TAMISEMI Datus Matuma,katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya afya ofisi ya rais TAMISEMI Deogratius Maufi.Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Siana Mapunjo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Wakuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba,Shinyanga Josephine Matiro na Kahama Fadhili Nkurlu wakiwa ukumbini
Mbele ni makatibu tawala wa wilaya ya Kishapu,Kahama na Shinyanga
Wenyeviti wa halmashauri za wilaya katika mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Kaimu Mkurugenzi Idara ya afya ofisi ya rais TAMISEMI Deogratius Maufi akizungumza wakati wa wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Mzabuni Teule “Prime Vendor System
Kushoto ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akiwa na Mkuu wa Masoko kutoka Bahari Pharmacy Limited Richard Olotu kutoka jijini Dar es salaam ambaye ndiye mzabuni mteule aliyeshinda kati ya wazabuni 14 walioomba kuwa wasambazaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika mkoa wa Shinyanga
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisaini mkataba kati ya mkoa wa Shinyanga na Mzabuni "Bahari Pharmacy Ltd" ambao watakuwa wasambazaji wakuu wa dawa katika vituo vya afya vya serikali mkoani Shinyanga
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisaini mkataba
Zoezi la kusaini mkataba linaendelea
Mwanasheria kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Lightness Tarimo akisaini mkataba huo
Zoezi la kusaini mkataba linaendelea
Mkuu wa Masoko kutoka Bahari Pharmacy Limited Richard Olotu kutoka jijini Dar es salaam akisaini mkataba
Viongozi wa halmashauri za wilaya wakisaini mktaba huo
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Stephen Magoiga akisaini mkataba huo
Viongozi wa halmashauri mbalimbali wakiendelea kusaini mkataba huo
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela (kushoto) akikabidhiana mkataba na Mkuu wa Masoko kutoka Bahari Pharmacy Limited Richard Olotu 
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje akichangia hoja ukumbini
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Jazia dawa,vifaa tiba na vitendanishi kwa kutumia mzabuni Teule Mmoja ‘Prime Vendor’
Uzinduzi unaendelea
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga akionesha mkataba baada ya uzinduzi
Kushoto ni Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli Kapologwe akipongezana na Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela baada ya uzinduzi
Uzinduzi umamelizika
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini......
Wadau wa afya wakiwa ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akizungumza baada ya uzinduzi huo
Meneja wa mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga Dr. Harun Kasale akizungumza ukumbini
Mwakilishi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Siana Mapunjo akiwa na Meneja wa mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga Dr. Harun Kasale
Katikati ni Meneja wa mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga Dr. Harun Kasale akisisitiza jambo
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli Kapologwe akiwa ukumbini
Mkuu wa Masoko kutoka Bahari Pharmacy Limited Richard Olotu akielezea namna alivyojipanga kuhakikisha kuwa dawa nyingi zinawafikia walengwa mkoani Shinyanga hivyo kuomba ushirikiano wa dhati kutoka kwa viongozi wa mkoa ili kufanikisha malengo yao.
Picha ya pamoja viongozi mbalimbali wa kitaifa,mkoa na wilaya za mkoa wa Shinyanga

Picha ya pamoja

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post