Jumapili Desemba 11,2016: Hapa ni katika kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga ambapo kambi ya vijana kanda ya Mashariki inayojumuisha halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Shinyanga na manispaa ya Shinyanga imefungwa.
Kambi hiyo iliyodumu kwa muda wa siku saba na kukutanisha vijana 180 wengi wao kutoka shule za msingi na sekondari imefungwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Akizungumza wakati wa kufunga Kambi hiyo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwataka vijana hao kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa pale wanapoona kuna dalili ya kufanyika uhalifu ikiwemo watu kuchoma moto shule.
Katika hatua nyingine aliwaasa vijana hao ambao hawapo shule kuunda vikundi vya ujasiriamali huku akiwataka viongozi wa skauti kuwa na ushirikiano wa karibu na halmashauri za wilaya wakae pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya kuimarisha chama cha skauti.
Akiwa katika kambi hiyo mkuu huyo wa wilaya alishuhudia mafunzo ya vijana wa skauti kwa vitendo ikiwemo kuvuka vikwazo.
Zoezi la kufunga kambi hiyo lilienda sambamba na zoezi la kumwapisha Luhende Richard Luhende kuwa mlezi wa skauti mkoa wa Shinyanga.
Tazama matukio katika picha wakati wa kufunga kambi hiyo
Vijana wa skauti wakiwa katika kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga wakisubiri kukaguliwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika uwanja wa zahanati ya Chibe katika katika kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga
Skauti wakijiandaa kukaguliwa.Wakiwa kambini vijana hao walikuwa wanashirikiana na wananchi wa kata ya Chibe kufanya usafi wa mazingira kama ilivyo kauli mbiu ya mheshimiwa rais John Pombe Magufuli
Maskauti wakimsubiri mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Kulia mbele ni Mlezi wa Skauti mkoa wa Shinyanga Luhende Richard Luhende akimwongoza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Skauti wakimwongoza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakatia akikagua skauti hao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(mwenye track suti nyeusi) akikagua vijana wa skauti mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(mwenye track suti nyeusi) akiteta na vijana wa skauti
Zoezi la ukaguzi linaendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(mwenye track suti nyeusi) akipanda mti katika zahanati ya Chibe iliyopo katika kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimwagilia maji mti alioupanda katika zahanati ya Chibe
Vijana wa skauti wakikimbia mchaka mchaka kuelekea katika pori la Chibe karibu na Bwawa la Ning'wa ambako ndiko walikuwa wameweka kambi ya siku 7
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kushoto) akikimbia mchakamchaka na vijana wa skauti kuelekea porini
Mchaka mchaka kuelekea porini
Skauti wakielekea porini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika kambi ya skauti kanda ya Mashariki katika kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga
Mlezi wa skauti mkoa wa Shinyanga Luhende Richard Luhende akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakipanda katika mawe yaliyopo katika pori la Chibe katika manispaa ya Shinyanga eneo ambao vijana wa skauti waliweka kambi ya siku 7
Kulia ni Naibu Kamishna Skauti mkoa wa Shinyanga Peter Mgalula akimwongoza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kuelekea katika pori la Chibe ambapo vijana wa skauti walikuwa wanafanyia mazoezi kwa vitendo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akielekea porini
Mratibu mkuu wa naibu kamishna Skauti mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mwita akimweleza jambo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Skauti akipanda mlima kwa kutumia kamba
Kijana akipanda juu ya mlima kwa kamba
Vijana wa skauti wakiwa juu ya jiwe kubwa baada ya kupanda kwa kutumia kamba ikiwa ni miongoni mwa mbinu za kuvuka vikwazo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia vijana hao
Ndani ya pori la Chibe
Vijana wakivuka kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa kutumia kamba juu ya miti
Kijana akipanda juu ya mti kwa kutumia kamba
Vijana wakipika chakula ndani ya bwawa la Ning'wa ikiwa ni mbinu inayotumika wakati wa mafuriko
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishuhudia vijana wakipika chakula ndani ya maji
Vijana wakiendelea kupika ndani ya maji
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoka katika bwawa la Ning'wa kuangalia mazoezi kwa vitendo ya vijana wa skauti
Mratibu mkuu wa naibu kamishna Skauti mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mwita akielezea namna wanavyotunza mazingira katika eneo la kambi yao
Kushoto ni mlezi wa skauti mkoa wa Shinyanga Luhende Richard Luhende,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na diwani wa kata ya Chibe wakiwa wamekaa juu ya kiti cha skauti
Kiti cha skauti kilichotengenezwa kwa miti
Vijana wa skauti wakionesha namna ya kupambana na adui
Jinsi ya kupambana na adui
Tunashuhudia yanayoendelea hapa kambini
Luhende Richard Luhende (katikati) akiapishwa kuwa Mlezi wa Skauti mkoa wa Shinyanga
Luhende Richard Luhende akiapa kuwa mlezi wa skauti mkoa wa Shinyanga
Luhende Richard Luhende akivalisha skafu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimpongeza Luhende Richard Luhende baada ya kuapishwa kuwa mlezi wa skauti mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimpongeza Luhende Richard Luhende baada ya kuapishwa kuwa mlezi wa skauti mkoa wa Shinyanga
Luhende akiendelea kupongezwa
Mratibu mkuu wa naibu kamishna Skauti mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mwita akisoma risala ambapo alisema madhumuni ya kambi hiyo iliyodumu kwa muda wa siku saba ni kuwaandaa na kuwajenga vijana kuwa wakakamavu na jasiri ili wajue namna ya kuishi katika mazingira ya kuheshimiana na kupendana kama kaka na dada.
Mratibu mkuu wa naibu kamishna Skauti mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mwita alisema skauti ni chama cha kielimu,malezi na michezo kwa vijana huku akielezea kuwa skauti ni neno la kiingereza lenye maana ya mtangulizi na mpelelezi ambaye kazi hasa ni kuona bila kuonekana akiwa ni mtiifu,mwaminifu,hodari na mwenye kushirikiana na wenzake
Mratibu mkuu wa naibu kamishna Skauti mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mwita alizitaja miongoni mwa changamoto zinazowakabili kuwa ni upungufu wa dawa za kutolea huduma ya kwanza,uhaba wa vifaa vya kutumia kambini,ukosefu wa mahitaji muhimu kambini ikiwemo chakula,mahema na mavazi,ukosefu wa ofisi ya skauti mkoa na ushirikiano mdogo baina ya maskauti na walimu wakuu wa shule kwa kutofuata waraka wa elimu namba 4 wa mwaka 2015 kuhusu kuhuisha na kuimarisha uskauti shuleni na vyuoni.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga kambi ya skauti kanda ya mashariki mwaka 2016 ambapo aliwataka vijana hao kuwa wazalendo wa nchi yao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga kambi ya skauti kanda ya mashariki mwaka 2016.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin