Mwakilishi wa baraza La habari Tanzania ( MCT) Shifaa Hassan ambaye ni afisa mwandamizi wa MCT kutoka Zanzibar akifungua semina ya kuhusu rejista (kanzi data) ya ukiukwaji wa uhuru wa wanahabari Tanzania (Press Freedom Violations Register -PFVR) iliyofanyika leo Jumatatu Desemba 19,2016 katika Hotel ya Nashera mjini Dodoma.
Washiriki wa semina hiyo pia wamejengewa uelewa juu ya matumizi ya kanzi data ya kurekodi matukio ya ukiukwaji wa uhuru wa habari.
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na waandishi wa habari mabalozi wa MCT kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara na visiwani wakiwemo baadhi ya wenyeviti wa klabu za waandishi wa habari katika mikoa
Wanahabari mabalozi wa MCT kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara na visiwani wakiwa katika mafunzo ya rejista ya ukiukwaji wa uhuru wa wana habari nchini
Mwakilishi wa baraza La habari Tanzania ( MCT) Shifaa Hassan akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo ambayo yalienda sambamba na mabalozi hao wa MCT kutoa ripoti za matukio ya ukiukwaji wa uhuru wa habari kutoka maeneo wanayotoka
Wanahabari mabalozi wa PFVR wakiwa katika warsha ya siku moja juu ya Rejista
Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia hotuba ya uzinduzi wa mafunzo hayo ya siku moja iliyofanyika hotel ya Nashera mjini Dodoma.
Washiriki wa mafunzo ya rejista ya ukiukwaji wa uhuru wa wanahabari nchini wakiwa katika mafunzo hayo mjini Dodoma
Mkufunzi wa mafunzo hayo bwana Brian kutoka studio 19 Ltd akitoa mafunzo ya utumiaji wa mitandao kutuma taarifa
Mwanzilishi wa Malunde1 blog na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga bwana Kadama Malunde akifuatilia mafunzo kwa vitendo.
Picha zote na Francis Godwin wa Matukiodaima blog
Social Plugin