Serikali
imeeleza dhamira yake ya kuongeza adhabu kwa watu wanaobainika kuhusika
na rushwa ili wawe wanalipa fidia ya hasara iliyojitokeza mbali na
kutumikia kifungo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mh. Angellah Kairuki
amesema kuwa adhabu zinazotolewa kwa wala rushwa ni ndogo ikilinganishwa
na hasara wanayoisababishia serikali, hivyo marekebisho ya sheria hizo
itamtaka mlarushwa kulipa fidia ya hasara iliyojitokeza
Akiongea
na waandishi wa habari, mara baada ya kuzinduliwa kwa wiki ya kupokea
malalamiko ya wananchi, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam, Mhe Angella amesema serikali itahakiki mali za viongozi wa
serikali wapatao 500 na kuwataka wananchi kujitokeza kuhakiki mali za
viongozi wao pamoja na kutoa taarifa ambazo serikali haikufanikiwa
kuzipata.
Social Plugin