ROBOTI WANAOWEZA KUSHIRIKI NGONO KAMA BINADAMU


Je ungependelea kushiriki ngono na roboti? ungefunga ndoa na roboti? na Je roboti anaweza kuwa na haki ya kupinga ndoa hiyo?

Haya ni baadhi ya maswala machache yanayoulizwa katika mkutano wa pili wa kuwa na mpenzi wa roboti mbali na kushiriki naye ngono katika chuo kikuu cha Goldsmith mjini London baada ya serikali ya Malaysia ambayo ndio iliokuwa taifa la maandalizi ya mkutano huo kuupiga marufuku.

Hatua hiyo imezua utata sio tu kwa mataifa yenye maoni ya Kihafidhina .


Ni watu wachache walioweza kusema kuwa roboti Pepe alikuwa na maumbile ya kuvutia

Hakukuwepo na wawakilishi kutoka kwa sekta ya ngono wala roboti za ngono katika mkutano huo.

Kampuni ya Real Dolls inayotengeza wanaserere wa ngono ilidai kwamba itatengeza roboti wa ngono aliye na akili bandia mwaka ujao.

Uzinduzi huo iwapo utafanyika utakuwa ushahidi wa David Levy ambaye amekuwa akitabiri ujio wa roboti zinazofanana na binadamu zenye akili bandia.

Alitoa hotuba ya kufunga mkutano huo ambapo alipendekeza utengezaji wa roboti za ngono.

''Tuna roboti za urafiki na sasa roboti ambaye anaweza kuwa mpenzi ndio mtindo mpya''.

Kwa wengine kushiriki ngono na roboti ni ndoto yao lakini kwa wengine ni uharibifu mkubwa

Katika kipindi cha miaka 10 ijayo, inawezakana kutengeza roboti ambayo watu wataihitaji kama mpenzi, ina upendo, inaaminika, inaheshima na hailalamiki alisema.

Wengi watapendelea uhusiano huo wa roboti na huenda wakataka kufunga ndoa nao.

Roboti inayoweza kushiriki ngono na binadamu huenda ikazinduliwa mwaka ujao

Mpango huo wa mpenzi wa aina ya roboti huenda akazua maswali kadhaa ya kimaadili, hususani wakati ambapo sheria italazimika kutambua roboti kama binaadamu.

Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post