Utafiti : MIMBA HUBADILISHA UBONGO WA MWANAMKE


Watafiti wanasema mwanamke anapokuwa na mimba, kiwango cha homoni ya oestrogen huongezeka sana na pia mwili wake kubadilika hata hivyo, si wataalamu wengi walikuwa wamechunguza mabadiliko kwenye ubongo.

Watafiti kutoka vyuo vikuu vya Universitat Autonoma de Barcelona na Leidenwalichunguza ubongo wa wanawake kabla ya kushika mimba, muda mfupi baada ya kujifungua na miaka miwili baadaye kuangalia mabadiliko kwenye ubongo. Matokeo ya utafiti wao yamechapishwa kwenye jarida la Nature Neuroscience.

Wanasayansi hao wanasema ujauzito hupunguza seli za ubongo katika baadhi ya sehemu za ubongo wa mwanamke ili kumuwezesha kuhusiana vyema zaidi na mtoto na kujiandaa kwa majukumu yake kama mama ambapo hubadilisha ubongo wa mwanamke kwa kipindi cha hadi miaka miwili.

Uchunguzi ulifanywa kwa wanawake 25 waliokuwa wameshika mimba kwa mara ya kwanza ulionyesha mabadiliko hayo kwenye ubongo hudumu kwa hadi miaka miwili baada ya mwanamke kujifungua.

Watafti hao wanasema vipimo vya sehemu tofauti za ubongo hubadilika kipindi hicho, sawa na inavyofanyika mtu anapovunja ungo, lakini hata hivyo, hawakupata ushahidi wowote wa kuathirika kwa uwezo wa mwanamke kuweka kumbukumbu.

Chanzo: BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post