WAHAMIAJI HARAMU 13 WANASWA WAKIFANYA BIASHARA YA UKAHABA DAR


Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imewakamata wasichana 13 kutoka nchi za Nebal na India wenye umri kati ya miaka 18 na 26 ambao wameletwa nchini kinyume cha sheria na kuendesha biashara ya ukahaba katika jijini humo.



Akiongea na waandishi wa habari leo mara baada ya kufanya oparesheni ya kufunga madanguro yote na kuwasaka raia wa kigeni wanaoishi nchini kinyume cha Sheria, Kamishna wa Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule amesema mbali na raia hao wa kigeni pia wamewamakata raia wa Kitanzania mbao wanashirikiana na wahamiaji hao.


Amemtaja Bwana Mohamed Shabani Magamba ambaye anatengeneza vibali vya kugushi ambapo pia amekutwa na pastpoti 4 za raia wa nchi za Nigeria, Botswana, Somalia na Uingereza.


Bwana Msumule ameitaja Wilaya ya Kinondoni kuwa inaongoza kwa kuwa na Madanguro ikifuatiwa na Temeke ambapo kwa sasa wanajipanga kuyaondoa kwa muda wa siku 10 madanguro hayo pamoja na kuendesha oparesheni kubwa katika Mitaa ya Msimbazi, Lumumba na Uhuru katika soko la Kariakoo na maeneo ya Mtoni Mtongani na Sabasaba ambako wamekwisha yafanyia uchunguzi wa kina.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post