Askari aliyekuwa akifanya kazi kituo kidogo cha polisi tarafa ya Igurubi wilayani Igunga mkoani Tabora, amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia shuka kutokana na kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Askari aliyejiua ametambulika kwa jina la G.4185 PC Geofrey Mwenda (32 ) ambaye inadaiwa hawara yake mpya ndiyo chanzo cha kuchukua maamuzi ya kutoa uhai wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamisi Issa alisema tukio hilo limetokea juzi saa tatu usiku.
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Issa alieleza kuwa askari huyo baada ya mke wake kusafiri, aliamua kuchukua uamuzi ya kuwa na mpenzi wa nje.
Alieleza askari huyo baadaye alikuja kugundua mpenzi wake ambaye hakuweza kumtaja jina lake, kuwa alikuwa na mwanaume mwingine mbali ya askari huyo.
Kutokana na ugunduzi huo ambao ulimfanya askari huyo achukie ndio alipoamua kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia shuka na kujining’iniza kwenye mti.
Na Robert Kakwesi, Mwananchi
Social Plugin