Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na ushindi katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Dimani, Zanzibar huku wakijizolea Kata nyingi za udiwani na kuwaacha mbali UKAWA.
CCM iliibuka na ushindi jimboni hapo baada ya mgombea wake Juma Ali Juma kupata kura 4,860 dhidi ya mpinzani wake wa UKAWA, Abdulrazak Khatib Ramadhani aliyejizolea kura 1,234.
Kwa upande wa UKAWA wamelalamikia uchaguzi huo wakisema kuwa uligubikwa na udanganyifu mkubwa kwani hata majina ya marehemu yalitumika kupigishwa kura.
Mgombe huyo wa CUF alisema kuwa dada yake ambaye amefariki tangu Januari 15 naye jina lake lilitumia katika kupigisha kura.
Jimbo hili la Dimani lilikuwa wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake, Hafidh Ally Tahri (CCM) kufariki Novemba mwaka jana akipatiwa matibabu mjini Dodoma.
Kwa matokeo ya Kata 13 yaliyokuwa yametolewa hadi leo asubuhi, CCM ilikuwa imeshinda udiwani katika Kata 12 huku CHADEMA ikiambulia Kata 1
Social Plugin