Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekiel Dibogo Wenje (Chadema 2010/15) amechaguliwa kwenye mkutano mkuu wa Kanda ya Ziwa Victoria, kuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda hiyo.
Wenje amemshinda Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Chief Kalumuna ambapo Uchaguzi huo umefanyika hii leo Januari 18,2017 Jijini Mwanza na matokeo yametangazwa hivi punde.
Katika uchaguzi huo, nafasi ya Makamu Mwenyekiti imeenda kwa Ansbert Ngurumo ambapo viongozi mbalimbali wa Chadema Taifa akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe, wamehudhuria mkutano.
Social Plugin