Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akizungumza wakati wa ukaribisho wa Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi walipotembelea ofisi za mamlaka hiyo.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakifuatilia maelezo ya awali ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) alipokuwa akitoa neno la ukaribisho.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya akizungumza wakati wa utamburisho wa Madiwani waliotembelea ofisi za MUWSA.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi aliyeongozana na Madiwani wa Halmashauri hiyo akizungumza wakati wa ziara ya madiwani katika ofisi za MUWSA.
Mkuu wa kitengo cha Mipango na Huduma za Biashara Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Tumaini Marandu akitoa taarifa ya Mamlaka hiyo kwa Madiwani waliofanya ziara katika ofsi za MUWSA.
Diwani wa kata ya Kilimanjaro,Priscus Tarimo akichangia jambo mara baada ya kusikiliza taarifa ya Mamlaka hiyo katika utoaji wa huduma ya maji safi na maji taka kwa wakazi wa manispaa ya Moshi.
Mkurugenzi ,Joyce Msiru akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizoibuliwa na madiwani katika kikao hicho.
Mkaguzi wa ndani wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Benson Maro akizungumza katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi(kushoto).
Madiwani wakiwa katika chanzo cha maji cha Shiri walipofanya ziara kutembelea vyanzo hicho na kupata maelezo.
Madiwani wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Ufundi wa Mamlaka hiyo ,Patrick Kibasa namna maji yanavyotibiwa.
Meneja Ufundi wa MUWSA,Patrick Kibasa akitoa maelezo kwa madiwani mara baada ya kutembelea chanzo cha maji cha Njoro ya Goha.
Madiwani wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) mara baada ya kuhitimisha ziara ya kutembea ofisi hizo pamoja na vyanzo vya maji.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Social Plugin