Jeneza lililofukuliwa likiwa halina kitu ndani yake |
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mbeya wakiwa wamelizunguka kaburi linalodaiwa kuzikwa jeneza bila mwili wa marehemu wakisubiri Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufukua kaburi ili kuhakikisha kama hakukuwa na mwili wa marehemu.
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mbeya wakiwa wamefurika kwenye makaburi ya Isanga ambapo kuna kaburi linalodaiwa kuzikwa jeneza bila mwili wa marehemu wakisubiri Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufukua kaburi ili kuhakikisha kama hakukuwa na mwili wa marehemu.Jeneza lililofukuliwa likiwa halina kitu ndani yakeMwenyekiti wa Mtaa wa Igoma pamoja na Baba wa Marehemu wakifunua jeneza kuhakikisha kama kulikuwa na mwili wa marehemuVijana wakiwa wanaondoa jeneza makaburini na kulipeleka kituo cha Polisi kwa ajili ya taratibu zingineJeneza baada ya kufukuliwa kutoka kaburiniKazi ya Kufukua kaburi ikiendelea
Wakazi wa eneo la Isanga katika jiji la Mbeya wameendelea kushuhudia visa na mikasa, ushilawadu na matukio ya vioja, baada ya mtoto wa miaka 9 aliyekuwa amezikwa jana kwenye makaburi ya Isanga kukutwa akiwa kitandani kwake amelala mara baada ya kurejea kutoka makaburini.
Mara baada ya kufika nyumbani familia ikiwa inaingia ndani mwao, walipigwa na butwaa baada ya kukuta mtoto wao amelala kitandani kwake, na baada ya kuitana na kumwamsha mtoto huyo aliamka na kuonekana akishangaa hali aliyoiona pale nyumbani.
TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha Mkoa wetu unakuwa mahala salama.
Kumekuwa na tukio 01 la taarifa ya kifo kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 16.01.2017 majira ya saa 10:30 Asubuhi huko Igoma “A”, Kata ya Isanga, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilipokea taarifa kuwa maiti iliyokwenda kuzikwa katika makaburini ya zamani ya Isanga kukutwa nyumbani, chumbani ikiwa kwenye godoro.
Kufuatia taarifa hiyo Polisi walifuatilia na kubaini kuwa tarehe 16.01.2017 majira ya saa 07:00 Asubuhi Mtu mmoja aitwaye JAILO KYANDO [36] Muosha magari na mke wake aitwaye ANNA ELIEZA [32] wote wakazi wa Mtaa wa Igoma “A” waliamka asubuhi na kukuta mtoto wao wa kwanza aitwaye HARUN JAILO KYANDO [09] amefariki dunia akiwa amelala.
Taarifa za awali zinadai kuwa marehemu tangu utoto wake alikuwa na matatizo ya ugonjwa wa kifafa hali iliyopelekea kuishi nyumbani pasipo kusoma. Kufuatia kifo hicho msiba uliendeshwa na taratibu za mazishi zilifanyika. Majira ya saa 12:00 Mchana jeneza lililoletwa msibani na kuwekwa sebuleni kando ya mwili wa marehemu ambao ulikuwa umeviringishwa na blanketi na kulazwa chini kwenye godoro, baada ya maombi yaliyoongozwa na walokole waitwao BONDE LA BARAKA vijana walibeba jeneza hadi makaburi ya zamani ya Isanga na kisha jeneza kuzikwa.
Waombolezaji waliporudi nyumbani walitaharuki kuona mwili wa marehemu Mtoto HARUN JAILO KYANDO ukiwa chumbani umelazwa eneo ulipokuwa awali. Kutokana na hali hiyo taarifa zilifikishwa Polisi mara moja, askari Polisi walifika na kurejesha hali ya amani kwa kuuchukua mwili wa marehemu ambao kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
****
Taratibu nyingine za mazishi zitafanyika leo tarehe 17.01.2017. Mpaka sasa bado haijafahamika ni uzembe /bahati mbaya wafiwa kusahau kuweka mwili wa marehemu kwenye jeneza au kulikuwa na hujuma zozote. Upelelezi unaendelea kuhusiana na tukio hili.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefika eneo la makaburi alipozikwa marehemu na kuongoza usimamizi wa ufukuaji wa kaburi hilo ulioanza majira ya saa Nne na nusu asubuhi hadi saa tano asubuhi.
Baada ya kumaliza kulifukua kaburi hilo vijana walilitoa jeneza kaburini ndipo Mwenyekiti wa Mtaa wa Igoma A, Fred Mwaiswelo alipofunua jeneza na kukuta ndani kukiwa tupu hali iliyoashiria mwili wa marehemu haukuwekwa ndani ya jeneza.
Kutokana na hali hiyo Jeshi la Polisi lilibeba jeneza hilo na kuelekea nalo katika kituo cha Polisi kati kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya kuwakabidhi ndugu kuendelea na taratibu za mazishi kwa mara nyine.
Hata hivyo baadhi ya ndugu na majirani wa Mtaa wa Igoma wamesema tukio hilo linaweza kuwa na sura mbili kwa maana hujuma kufanywa kwa maksudi au bahati mbaya ya kuusahau mwili wa marehemu.
Wamesema inaweza kuwa hujuma kutokana na kawaida ya misiba kabla ya mazishi lazima ndugu watoe heshima za mwisho kwa marehemu lakini kwa msiba huo haikufanyika pamoja na baadhi ya ndugu kutohudhuria mazishi ya marehemu.
Chanzo-Mbeya yetu blog
Social Plugin