Mbwa huyo wa umri wa wiki 12 kwa jina Macie, alikimbizwa kwa daktari wa mifugo kwa huduma ya dharura baada ya kuanza kukohoa.
Mwenye mbwa huyo anasema alidhani kuwa alikuwa amemeza kifaa cha kuchezea cha watoto, lakini X ray baadaye ilionyesha picha ya kisu kikuwa tumboni.
Daktari ambaye amekuwa akimtunza mbwa huyo tangu afanyiwe upasuaji anasema ana bahati sana kuwa hai.
Mwenye mbwa huyo kutoka Glasgow alikuwa amempoteza mbwa wake mwingine kutokana na ugonjwa wa saratani
Siku moja baada ya kufanyiwa upusuaji alionekana mchangamfu. Mbwa huyo amekuwa akirudishwa kwa daktari kufanyiwa ukaguzi kwa muda wa wiki mbili na sasa anaendelea kupata nafuu.
Social Plugin