Leo Ijumaa Januari 13, 2017 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kipolisi Kinondoni imetoa taarifa ya kumkamata Samson Mahimbo mkazi wa Makongo Juu Dar es salaam ambaye ni Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) kwa tuhuma za rushwa ya ngono dhidi ya mwanafunzi wa chuo hicho.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, Denis Manumbu mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuwekewa mtego kutokana na taarifa iliyotolewa na mwanafunzi aliyeombwa rushwa hiyo ili aweze kumpatia matokeo mazuri ya mtihani wake wa marudio (Supplementary Exams).
“Bwana Mahimbo alimtaka mtoa taarifa (Mwanafunzi) kufika katika Bar ya Shani iliyoko maeneo ya Sinza jirani na Bar ya Meeda na alitii agizo hilo ambapo walikutana na akapewa majibu ya mtihani wa somo la Road Transport, na kuyaandika ili arekebishe mtihani wake alioufanya Janury 5, 2017”,alesema Manumbu
Baada ya marekebisho hayo mtuhumiwa pamoja na mtoa taarifa walielekea katika nyumba ya kulala wageni ya Camp David na kuingia katika moja ya vyumba vya nyumba hiyo, wakati akiwa tayari ameshajiandaa kwaajili ya kutekeleza azma yake ya kumuingilia kimwili mtoa taarifa, ndipo alikamatwa na maafisa wa TAKUKURU” ,aliongeza.
Social Plugin