Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonald Masalle, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, akifungua Kongamano la Maaskofu wa Jumuiya ya Makanisa ya Kiinjilisti Ulimwenguni Agape WUEMA kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, linalofanyika kwa siku mbili (leo na kesho) Jijini Mwanza.
Kongamano hilo limelenga kujadili na kuazimia mgawanyo wa ujenzi wa miradi ya jumuiya hiyo katika nchi sita za Afrika Mashariki na Kati (Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Kongo) ambayo ni pamoja na Makanisa, Shule na Hospitali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa mataifa husika.
Aliyesimama kulia ni Askofu Mkuu wa Agape WUEMA barani Afrika, Mande Wilson, akizungumza kwenye kongamano hilo.
Askofu Mkuu wa Agape WUEMA Tanzania, Martin Gwilla, akizungumza kwenye kongamano hilo
Maaskofu mbalimbali wa jumuiya ya Agape WUEMA kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na Kati
Binagi Media Group
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na taasisi hizo.
Hayo yamebainishwa katika risala yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonald Masalle kwenye ufunguzi wa kongamano la Maaskofu wa Jumuiya ya Makanisa ya Kiinjilisti Ulimwenguni AGAPE WUEMA kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, linalofanyika Jijini Mwanza.
Amesema serikali inaunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na jumuiya hiyo katika kufanikisha utekelezaji wa miradi yake nchini ikiwemo ujenzi wa makanisa, shule pamoja na hospitali.
Askofu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Martin Gwila, ameishukuru seikali kwa ushirikiano wake ikiwemo kuruhusu ujenzi wa miradi iliyokusudiwa ambapo ameomba ushirikiano huo kuwa endelevu kwani miradi hiyo itaongeza chachu ya maendeleo katika jamii.
Askofu Mkuu wa Jumuiya ya AGAPE WUEMA barani Afrika, Mande Wilsoni, amebainisha kwamba kongamano hilo lililowakutanisha zaidi ya Maaskofu 170 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati limenga kuhakikisha ugawaji na utekelezaji wa miradi iliyokusudiwa unaanza mapema mwaka huu.
Social Plugin