Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga akiwasalimia wachimbaji 15 wa madini ambao walikuwa wamefukiwa na kifusi kwenye Mgodi wa RZ,katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.Picha zote kwa hisani ya Joel Maduka wa Madukaonline blog
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga,akitaniana na wachimbaji hao.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga,akisalimiana na raia wa China.
Mchungaji wa kanisa la FPCT Geita Mathias Gundula ,Akimshukuru Mungu juu ya yale ambayo ameyateda kwa vijana ambao wameokolewa kutoka mgodini.
Mganga mfawidhi wa Hospital ya mkoa wa Geita Dk. Brian Mawalla akimwakikishia mkuu wa mkoa kuwa vijana wapo salama na wanaweza kwenda kuendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa
Mwanasheria wa mgodi huo,Francis Kiganga,akimkikishia mkuu wa mkoa kutekeleza maagizo yote ambayo wamepatiwa.
Mwanasheria wa mgodi huo,Francis Kiganga akionesha ramani ya shimo mbele ya waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali.
Mchimbaji akimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa jitihada ambazo zimefanyika na wao kutoka wakiwa hai.
*****
Wachimbaji 15 wakiwemo watanzania 14 na raia mmoja wa China walionusurika na kifo baada ya kuokolewa kutoka chini ya ardhi kwenye mgodi wa dhahabu wa RZ Union ulioko kijiji cha Mawemeru kata ya Nyarugusu mkoani Geita baada ya kukaa siku 3 bila chakula wala huduma yoyote wameruhusiwa kutoka HospitalI ya mkoa wa Geita walikopelekwa kupata matibabu.
Akiwaaga baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali mkuu wa mkoa wa huo,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,amewaomba kurudi na kuendelea kujituma katika shughuli ambazo wanafanya ili kuendelea na ujenzi wa taifa.
“Mko imara sasa mrudi mkaendelee tena na ujenzi wa taifa letu shughuli hizi ndiyo zitawasaidia kupata kipato tumefarijika sana miongoni mwenu hayupo hata mmoja aliyeteteleka”,alisema Kyunga.
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amesema kuwa wamekubaliana na mgodi huo wafanyakazi wote katika mgodi huo kupatiwa mkataba ambao utawasaidia wafanyakazi na pia amewaomba kuwa na mahusiano baina ya wafanyakazi na waajili ambo ni raia wa china na pia amewasisitiza kumrudia Mungu kwani amewanusuru na kifo.
Aidha kwa upande wake Mwanasheria wa mgodi huo,Francis Kiganga pamoja na kuyashuru mashirika ambayo yamejitolea kufanya shughuli za uokoaji pia amemkikishia mkuu wa wilaya kuongeza mkataba wa kazi badala ya miezi mitatu atawapa wa mwaka mzima.
Akiwaruhusu wahanga hao, mganga mfawidhi wa Hospital ya mkoa wa Geita Dk. Brian Mawalla amesema wamefikia uamuzi wa kuwaruhusu baada ya kujiridhisha na maendeleo mazuri ya afya zao.
Wachimbaji hao ameokolewa Januari 29 mwaka huu kwa msaada kutoka makampuni ya Busolwa Mining,Nyarugusu,GGM na ACACIA ,waliofukiwa na udongo wa kifusi cha mgodi huo Januari 26 mwaka huu.