Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametishia kuyafuta magazeti mawili nchini aliyodai yamekuwa yakiandika habari za uchochezi.
Rais Magufuli ameyasema hayo mjini Shinyanga wakati akifungua kiwanda cha Jambo Food Products Co. Ltd kinachojihusisha na uzalishaji wa vinywaji mbalimbali ikiwemo maji,soda na juisi na kiwanda cha Fresho Investment Co.Ltd PP Bags Factory kinachojihusisha uzalishaji wa vifungashio vya bidhaa mbalimbali.
“Navipongeza sana vyombo vyote vya habari kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuhabarisha watanzania,nazipongeza Televisheni zote,nayapongeza magazeti yote isipokuwa magazeti mawili tu ambayo yenyewe kila siku ni kuandika habari za uchochezi tu,bahati nzuri watanzania wanayajua na mara wamekuwa wakipuuza habari zao,wao ukizungumza neno wanageuza neno hili”,amesema rais Magufuli.
“Magazeti haya mawili siku zao zinahesabika,huo ndiyo ujumbe wasifikiri wanafanya tunawaangalia,serikali ya kutumbua majipu haiwezi kuacha kutumbua magazeti yanayofanya kazi ya kuchochea,kama wanasikia wasikie,kama hawasikii wasisikie”,amesema.
Msikilize Hapa rais John Pombe Magufuli akitishia kuyatumbua magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi
Social Plugin