Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kuwasili mkoani Shinyanga Januari 12,2017 kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kuwasalimia wananchi wa mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza na waandishi wahabari leo mchana,mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amesema rais Magufuli atazungumza na wakazi wa Shinyanga siku ya Alhamis mchana Januari 12,2017 katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Mkuu huyo wa mkoa amewaomba wakazi wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kumpokea mheshimiwa rais.
Maadhimisho ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar kitaifa yatafanyika Zanzibar.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumatatu Januari 9,2017-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Waandishi wa habari wakiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo mchana Januari 9,2017
Waandishi wa habari wakiwa ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza na waandishi wa habari
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin