Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tanzia: MWANDISHI WA HABARI AMINA ATHUMANI AFARIKI DUNIA,ALIKUWA ZANZIBAR KURIPOTI MAPINDUZI CUP



Amina Athumani enzi za uhai wake
Mwandishi wa habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru na Mzalendo, Amina Athuman amefariki dunia leo asubuhi Jumapili Januari 15,2017 katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar alikokuwa amelazwa.


Amina alilazwa Hospitalini hapo baada ya kuzidiwa (kushikwa na uchungu) kutokana na ujauzito na kukimbizwa kupata huduma katika hospitali hiyo ambapo alijifungua mtoto wa kiume (bahati mbaya) na yeye akaendelea kupatiwa matibabu hadi umauti ulipomkuta leo asubuhi.

Amina alikuwa mjini Zanzibar kikazi alipokwenda kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo alikuwa arejee jijini Dar es Salaam jana.

Msiba wake upo jijini Dar es salaam.

Mungu ilaze roho ya Marehemu Amina Athuman mahala pema peponi Amina

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com