Kufuatia tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda zikiwahusisha baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi Askari 12 waliotuhumiwa ili uchunguzi ufanyike dhidi yao.
Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi uliopita, IGP Mangu alisema ni lazima Jeshi la polisi lichukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo, hata kama ni askari.
"Jeshi la Polisi linachukua hatua madhubuti za kuwachunguza Askari na Wasanii wote waliotuhumiwa na baada ya uchunguzi kumamilika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayethibitika kwa uhalifu huo"alisema IGP Mangu.
Pia IGP Mangu ameiomba jamii kuendelea kutoa taarifa za uhalifu wa aina yeyote ili nchi iendelee kuwa salama. Hapo chini ni Majina ya Askari wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya, ambao wamesimamishwa kazi.
Social Plugin