Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JINSI MKALIMANI ALIVYOKAMATWA AKITAFSIRI VISIVYO MANENO YA MTALII TANZANIA

Mkalimani katika mbuga ya wanyama pori nchini Tanzania amekamatwa baada ya kutafsiri visivyo matamshi ya mtalii mmoja kuhusu nchi na watu wake.

Kwenye video iliyosambazwa kwa wingi katika mitandao ya kijamii, mkalimani huyo anasema kuwa mtalii huyo anataka watu wa Tanzania waache kulalamika kwa sababu ya njaa wanaweza kula hata maua.
Ukweli ni kwamba mwananke huyo anasema kuwa watanzania ni wazuri kupindukia.
Alikamatwa siku ya Alhamisi kwa agizo la waziri wa utalii.
Mkalimani huyo ambaye hakutajwa jina ni kutoka mbuga ya Serengeti iliyo kaskazini magharibi mwa nchi.
Kamanda wa polisi eneo hilo Philipo Kalangi, alisema kuwa anahojiwa lakini hakutoa habari za kina.
Inaelezwa kuwa huenda waziri alihisi kuwa mkalimani huyo alikuwa akimsuta mtalii au alikuwa akimuiga Rais John Magufuli.
Katika Video hiyo, mtalii anasema:
"Hii  Ziara yangu nchini Tanzania imekuwa nzuri,watu ni wazuri na wenye urafiki,Salamu kwa kawaida ni Jambo, nina furaha kuwa hapa, ardhi ni nzuri."
Mkalimani anatafsiri hivi:
"Anasema watanzania mnalia sana njaa, kila siku mnalia njaa wakati mna maua nyumbani, si mchemshe maua mnywe, anasema si vizuri kulia njaa."
Mtalii
"Aina nyingi ya wanyama na watu unaona ni wazuri, kinyume na sehemu zingine. Ni nzuri."
Mkalimani
"Anasema mnamuomba rais wenu awapikie chakula, kwani rais wenu ni mpishi, hangaikeni mfanye kazi,chemsheni hata nguo mnywe."
Mtalii
"Ni kitu mabacho utakikumbuka katika maisha yako yote. Ni nzuri na ni ya kupendeza."
Mkalimani
"Anasema mhangaikeni pembezoni za nchi, muache rais hawezi kutoka Ikulu akuje kuwapikia chakula, hivyo mjipikie wenyewe."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com