Kamati ya kongamano ya vyuo vikuu Shinyanga, wakishirikiana na Mwalimu Happiness Mathew Kihama ( Mkurugenzi mtendaji wa EASYFLEX PRODUCTION), wanakuletea Kongamano kubwa la maombi kwa wanavyuo wote Shinyanga litakalofanyika siku ya Jumamosi February 11,2017 katika chuo kikuu cha ushirika Moshi cumpus ya Kizumbi kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni.
Mgeni rasmi katika kongamano hilo atakuwa Mheshimiwa Josephine Matiro, mkuu wa wilaya ya Shinyanga mjini. Mambo hayo yataongozwa na Mwalimu Happiness Mathew Kihama.
KAULI MBIU: Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa. mithali 1: 7
Kwaya mbalimbali na waimbaji binafsi kutoka Shinyanga watakuwepo, pia kutakuwepo na vipindi vya kusifu na kuabudu sambamba na maombi mazito ya kuvunja ngome za muovu shetani.
Kwa mawasiliano zaidi, piga simu
1. 0754266396 - Msimamizi
2. 0756801641 - MOCU
3. 0768923256 - Kolandoto
4. 0765055854 - Shycom
5. 0764988339 - Vijana centre
6. 0769973241 - Veta
WATU WOTE MNAKARIBISHWA!!
Social Plugin