Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAKONDA AANIKA MAJINA YA VIGOGO SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA..ANGALIA MAJINA 65 HAPA


Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam,Paul Makonda amewataja watuhumiwa 65 wa Dawa za Kulevya,katika majina hayo ametajwa Freeman Mbowe,Mchungaji Gwajima,Yusuf Manji,Idd Azzan.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake mapema leo jijini Dar,RC Makonda ameingia katika awamu ya pili ya kutaja majina hayo na kuyaweka hadharani.

Katika hatua nyingine RC Makonda amekiri kukamatwa kwa Mmiliki wa kituo cha Radio ya EFM,ajulikanae kwa jina la Francis Ciza,almaarufu kwa jina la Dj Majay. 

"Tulipokuwa tukifanya opereseheni ya kuwakamata Wahusika weote wa Dawa za kulevya juzi usiku nae akakamatwa kws mahojiano zaidi",alisema Makonda.

Makonda amejibu habari za kukamatwa kwa Dj Majay mara baada ya kuulizwa swali na mmoja wa waandishi wa habari,kufuatia tetesi nyingi zilizokuwa zikisambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Makonda amewataka watu wote 65 waliotajwa, kuhakikisha wanaripoti kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Sentro) siku ya Ijumaa saa 5 asubuhi kwa mahojiano zaidi.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Makonda amesema kuwa, waliokamatwa awali ndiyo waliofanikisha kupatikana kwa orodha hiyo mpya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com