Vita hiyo juu ya madawa ya kulevya imefika mpaka bungeni na baadhi ya wabunge walikuwa wakitoa hoja mbalimbali huko mjini Dodoma.
Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga jana alisema yeye yupo tayari kuwataja baadhi ya wabunge wanaohusika na biashara hiyo.
Mbunge huyo awali alizungumzia mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya elimu lakini la mwisho aliweza kuzungumzia suala hilo ambalo kwa sasa kila mtu anataka kutambua nini kinaendelea.
” Suala ninalotaka ni hili suala linashika headline ni suala la madawa ya kulevya, naomba niwaambie sisi viongozi naomba niquote, ‘nitasema ukweli uongo kwangu mwiko.’ Kwahiyo nitakachotaka kukisema mtu yeyote akitaka anihukumu akihukumu chama changu kwanza, na kama wewe ni mwana CCM utanichukia rudisha kadi ndo unichukie.
"Wafanya biashara wa madawa ya kulevya hakuna asiowajua, tunawajua humu ndani wapo, nje ya bunge wapo, kwanini hatuwataji?"alihoji.
Aliongeza, “Kwanini hatuwataji tunakaa kimya? Mheshimiwa mwenyekiti kama kwa ridhaa yako unaniruhusu mimi nitawataja hata humu ndani. Madawa ya kulevya ni pamoja na bangi, kuna mbunge alisimama humu alisema bangi hazina madhara alijuaje kama hazina madhara kama hatumii? tungeanza na huyu.
"Viongozi wenzangu naomba niwahakikishie kama tutakuwa wanafiki mbinguni sisi ndiyo tutakaokuwa kuni, tutakuwa kuni mbinguni tunawafumbia macho watumiaji wa madawa ya kulevya tunakula nao.
"Nimpongeze ndugu yangu Paul Makonda kwa kuthubutu kutaja neno madawa ya kulevya lakini nimhakikishie kila marafiki watano wanaomzunguka watatu ni wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, aanze na hao.”
Social Plugin