Mkalimani anayedaiwa kutafsiri maneno yasiyo sahihi kutoka kwa mmoja wa watalii aliyetembea hifadhi ya Ngorongoro, hatimaye ameibuka na kuomba radhi kutokana na video hiyo iliyosambaa kwa madai kuwa alikuwa katika mazingira ya kufanya utani.
Awali mkalimani huyo anayeitwa Simon Sirikwa aliwekwa chini ya ulinzi kutokana kile kilichokuwakinatafsiriwa kudaiwa kuwa kilikuwa kinapotosha uhalisia wa maneno yaliyokuwa yakizungumzwa na mtalii aliyekuwa akisifia kile alichokiona baada ya kutembelea eneo hilo la utalii.
Hata hivyo katika video mpya aliyoitoa akiwa na mtalii yule yule aliyeonekana katika video ya kwanza, amesikika akizungumza kwa lugha ya Kiswahili akiomba radhi kwa kile alichokuwa amezungumza kwenye video ya awali.
"Kama mlivyoona video yangu niliyopitisha mimi ni tour guide kwa zaidi ya miaka kumi sasa, siwezi kuichafua hii nchi hata kidogo, hata aliyetoa hiyo video kwenye Facebook, kwenda kwenye Whatsapp na kuisambaza kwenye makundi ya kijamii atakuwa amekosea," amesema Sirikwa.
"Lakini ilikuwa ni comedy, ilikuwa ni utani, na najua kuna watu wamekwazika, ila naomba samahani kwa waliokwazika, ila kwa mafansi wangu, wafuasi wangu endeleeni kupata burudani, ila mfahamu sijafanya hichi kitu kwa serious wala sikuwa na makusudio yoyote mabaya, asanteni."
Baadhi ya watu wanaomfahamu Sirikwa walipohojiwa na BBC wamemuelezea alivyo mtu wa utani na kwamba anajulikana kwa jina la utani kama Mpondam
Haijabainika iwapo Sirikwa aliachiliwa huru bila masharti au aliachiliwa huru kwa dhamana.
Mwanamke mtalii kwenye video hiyo ya pili anasikika akisema: "Hamjambo tena, Sehemu ya pili ya video yetu. Tunacheza tu. Simon alikuwa anafanya ucheshi tu na tulikuwa tunafanya utani tu kidogo kwenye Facebook.
Ijumaa, kamanda wa polisi wa kanda hiyo Jaffari Mohammed aliambia BBC kwamba mwelekezi huyo alikuwa "amempotosha" mtalii huyo na kwamba polisi walikuwa wakifanya uchunguzi kubaini iwapo alisambaza video hiyo mitandao ya kijamii kinyume na sheria za uhalifu wa kimitandao.
Sheria hiyo inatoa faini ya kuanzia $1,300 (£1,000) na kifungo cha kuanzia miezi mitatu jela kwa anayepatikana na kosa la kuchapisha habari za uongo, za kuhadaa au za kupotosha kwa kutumia kompyuta.
Sheria hiyo ilianza kutekelezwa mwaka 2015.
Mwelekezi huyo alikamatwa kwa azigo la Waziri wa Utalii Jumanne Maghembe.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam anasema kuwa huenda waziri alihisi kuwa mkalimani huyo alikuwa akimsuta mtalii au alikuwa akimuiga Rais John Magufuli.
Kwenye video hiyo asili, mtalii anasema:
"Hi. Ziara yangu nchini Tanzania imekuwa nzuri. watu ni wazui na wenye urafiki. Salamu kwa kawaida ni Jambo, nina furaha kuwa hapa, Ardhi ni nzuri."
Mkalimani anatafsiri hivi:
"Anasema watanzania mnalia sana njaa, kila siku mnalia nja wakati mna maua nyumbani, si mchemshe maua mnywe, anasema si vizuri kulia njaa."
Mtalii
"Aina nyingi ya wanyama na watu unaona ni wazuri, kinyume na sehemu zingine. Ni nzuri."
Mkalimani
"Anasema mnamuomba rais wenu awapikie chakula, kwani rais wenu ni mpishi, angahikeni mfanye kazi,chemsheni hata nguo mnywe."
Mtalii
"Ni kitu mabacho utakikumbuka katika maisha yako yote. Ni nzuri na ni ya kupendeza."
Mkalimani
"Anasema mhangaikeni pembezoni za nchi, muache rais hawezi kutoka Ikulu akuje kuwapikia chakula, hivyo mjipikie wenyewe."
Via>>BBC
Social Plugin