Mke wa Rais mkongwe wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amesema kuwa mumewe ni mashuhuri sana hivi kwamba anaweza kupigiwa kura hata akiwa maiti.
Bwana Mugabe, ambaye atakuwa na umri wa miaka 93 mnamo Jumanne, ametangaza mara kadhaa kuwa atagombea kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Grace Mugabe ana miaka 40 mchanga kwa mumewe.
Aliambia mkutano wa chama tawala cha ZANU-PF kuwa hata mumewe akifariki, bado jina lake litawekwa kwenye karatasi za kupiga kura.
Alisema watu wa Zimbabwe wanampenda rais wao sana, hivi kwamba wangempigia kura hata akiwa maiti.
Bi Mugabe amekuwa mkosoaji mkuu wa wakosoaji wa mumewe na kwa wale walio na tamaa ya kumrithi.
Inadhaniwa kuwa alikuwa mstari wa mbele wa kumwachisha kazi aliyekuwa makamu wa rais, Joice Mujuru mwaka 2014.
Bwana Mugabe, ambaye siku hizi haonekani sana hadharani, ametawala Zimbabwe tangu taifa hilo kuwa huru miaka 37 iliyopita.
Via>>BBC
Social Plugin