Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha 46- MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA TANZANIA YALIVYOFANYIKA MKOA WA SHINYANGA


Alhamis Februari 2,2017-Hapa ni katika viwanja vya Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga ambako kumefanyika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini Tanzania inayoashiria uzinduzi wa mwaka mpya wa Kimahakama.


Kauli mbiu ya Siku ya Sheria nchini Tanzania Mwaka huu 2017 ni "Umuhimu wa utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi".

Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo/maadhimisho ya siku ya sheria "Law Day" alikuwa kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Kahama Fadhili Nkurlu ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kahama.

Pamoja na mambo kadha wa kadha yaliyojiri wakati wa maadhimisho hayo,kilio kikubwa cha wadau wa mahakama kilikuwa ni umuhimu wa mahakama kutoa haki kwa wakati kwani uchelewashaji wa utoaji haki unawafanya wananchi washindwe kufanya shughuli za maendeleo matokeo yake kurudisha uchumi wa nchi nyuma.

Lawama nyingi zilitupwa kwa jeshi la polisi kuwashikilia watuhumiwa kwa muda wa zaidi ya saa 24 bila kuwafikisha mahakamani lakini pia polisi kukwamisha kesi mahakamani kwa kuchelewa kupeleka ushahidi mahakamani.

Mahakama nayo inakanyoshewa vidole kwa baadhi ya majaji,mawakili wa serikali,makarani na mahakimu kuendekeza rushwa,wananchi kutopewa nakala za kesi zao kwa wakati huku wananchi nao wakilaumiwa kwa kutotoa ushirikiano mahakamani.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,KadamaMalunde,alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha 46 za Matukio yaliyojiri...Tazama hapa chini
Wa kwanza kushoto ni Profesa jaji John Ruhangisa wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga,mgeni rasmi kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Fadhili Nkurlu na Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Richard Kibela
Meza kuu
Kushoto ni Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Richard Kibela akiteta jambo na Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Victoria Makani
Wa kwanza kushoto ni Wakili wa serikali mkuu mfawidhi Shinyanga Pendo Makondo akifuatiwa na mkuu wa wilayaya Shinyanga Josephine Matiro akifuatiwa na Profesa jaji John Ruhangisa wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Fadhili Nkurlu akiteta jambo na Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga
Sheikh mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya akiomba dua wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini
Askofu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Emmanuel Makala akiombea mahakama za Tanzania
Mahakimu na watumishi wa mahakama wakiwa eneo la tukio
Askofu wa kanisa la Anglikana akiomba dua/sala
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT),Dayosisi ya Shinyanga, Dkt. John Nkola akiombea mahakama iwe kitovu cha haki na majaji na mahakimu kuwa na hofu ya mungu katika kutoa haki
Meza kuu wakiomba
Askofu wa kanisa la EAGT akiomba
Kushoto ni Mchungaji wa kanisa la SDA akiomba
Kiongozi wa dini akiomba
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Fadhili Nkurlu akiteta jambo na Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga
Watumishi wa mahakama wakiwa eneo la tukio
Watumishi wa mahakama 
Mahakimu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE John Myola (aliyevaa miwani) akiwa eneo la tukio
Mgeni rasmi Fadhili Nkurlu (katikati) akitafakari jambo
Tunafuatilia kinachoendelea....
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Waaandishi wa habari wakiwa eneo la tukio
Askari polisi wakiwa eneo la tukio
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Tunafuatilia kinachoendelea.....
Watumishi wa mahakama na mawakili
Kaimu mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea mkoa wa Shinyanga Paul Kaunda akizungumza ambapo alisema nakala za hukumu hazichapwi kwa wakati na hata zikichapwa mahakimu wamekuwa wakitumia muda mrefu kuzifanyia uhakiki hivyo kuchelewesha azma na haki yam kata rufaa katika mahakama za juu.
Kaunda alisema utoaji wa haki kwa wakati utasaidia kwa kiasi kikubwa kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali hapa nchini
Wakili wa serikali mkuu mfawidhi Shinyanga Pendo Makondo akizungumza ambapo alisema endapo kesi zitaisha kwa wakati mahakamani itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi kwani wananchi watafanya shughuli zao badala ya kuwaza kesi kila siku
Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Richard Kibela akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini.Jaji Kibela alisema katika kipindi cha mwaka 2016 mahakama hiyo iliamua jumla ya mashauri 392 yakiwa ni kati ya mashauri yaliyokuwa yamefunguliwa na yake yaliyobaki mwaka 2015 ambayo kwa ujumla yalikuwa mashauri 1087.
Jaji Kibela alisema kesi nyingi zimerithiwa kutoka mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Tabora kabla ya kuanzisha kanda hii mwaka 2015 
Mgeni rasmi/Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Fadhili Nkurlu akiwahutubia wadau wa mahakama ambapo aliisisitiza mahakama kutoa haki kwa wakati ili wananchi waweze kufanya shughuli za maendeleo kuinua uchumi wa nchi
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Fadhili Nkurlu aliwaomba watanzania kuwapuuza baadhi ya watu wanaosema kuwa mahakama zinaingiliwa kimajukumu
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Fadhili Nkurlu
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha watu wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner akifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Picha ya pamoja,mgeni rasmi,majaji ,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga na viongozi wa dini
Picha ya pamoja,mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili  na viongozi wa dini
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili  na mahakimu
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji ,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili na mawakili wa serikali na wa kujitegemea
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili  na viongozi wa taasisi mbalimbali
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili  na watumishi wa mahakama
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili watumishi wa mahakama na wadau wengine wa mahakama
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili  na wadau wa mahakama
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili na waandishi wa habari
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com