Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima(TEWW) imetoa onyo Kwa vituo 155 vinavyofundisha elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi na kuwa vipo kwenye hatari ya kufutiwa usajili.
Akizungumza jana Dar es Salaam Naibu Mkurugenzi TEWW, Dk Kassim Nihuka alisema idadi ya vijana na watu wazima waliokosa elimu ya sekondari imeongezeka hapa nchini na nchi zote za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Alisema hadi sasa Kuna vituo 337 vinaendeshwa na wadau na 83 vinaendeshwa na Serikali nchi nzima.
"Katika vituo vya elimu ya Watu wazima 337 ambapo 182 vina usajili na 155 vina usajili lakini vinakiuka matakwa yaliyowekwa na vipo kwenye hatari ya kufutiwa usajili pia ambavyo havijasajiliwa bado hatujafanya utafiti vipo vingapi," alisema Dk Nihuka.