Wenye vipara wakishiriki katika mchezo wa kuvutana na kamba Japan
***
Zaidi ya wanaume 30 wenye vipara kichwani nchini Japan wanaadhimisha siku kuu yao ya kila mwaka inayoshirikisha mchezo wa kuvuta kamba.
Klabu hiyo ya wenye vipara inawajumuisha wananchama 65 kutoka maeneo tofauti nchini tangu ibuniwe 1989.
Lengo ni kuwahamasisha watu zaidi kuhusu watu wenye vipara
Mwanachama wa watu wenye vipara akishiriki katika mchezo wa kuvutana kwa kutumia kamba Japan
Mwenyekiti wa klabu hiyo Teijiro Sugo mwenye umri wa miaka 70 alisema kuwa matumaini ni kwamba klabu hiyo ingewavutia wanachama zaidi na kuwa kubwa zaidi.
''Nawataka wanaume wote walio na upara duniani kukongamana hapa ili kuanzisha michezo ya olimpiki'',alisema.
Social Plugin