Mwanamume mmoja amefariki baada ya kupigwa na umeme alipokuwa alichaji simu yake huku akioga kwenye bafu.
Richard Bull, mwenye umri wa miaka 32 alifariki wakati chaji yake ya aina ya iphone ilipoguza maji aliyokuwa akioga nyumbani kwake huko Ealing, mashariki mwa London.
Kifo chake kilitajwa kama kilichotokana na ajali.
Makundi ya kampeni yamekuwa yakiwashauri watu wasichaji simu karibu na maji.Bwa Bull alikuwa akichaji simu yake wakati alipigwa na umeme
Alipata majeraha ya moto kifuani, na kwenye mkono wake wakati kifaa hicho kilipokaribiana na maji tarehe 11 mwezi Disemba.
Kisa hicho kimechangia kuangaziwa kwa hatari zinazosababishwa na vifaa vya umeme hasa wakati viko karibu na maji.
Idara ya usalama unayosika na kuzuia ajali inawaonya watu ikiwataka wasitumie vifaa vya umeme kwenye bafu.
Chanzo-BBC
Social Plugin