Mkazi wa Tazara Magorofani, Shaban Biro (47), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ,jijini Dar es salaam kujibu shtaka la kusambaza na kuonyesha picha za utupu katika mitandao ya kijamii.
Biro (47), alifikishwa mahakamani hapo leo na kusomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Flora Mjaya.
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Glory Mwenda, alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa Machi, 2016 mtaa wa Kilosa uliopo wilaya ya Ilala.
Inadaiwa mshitakiwa alisambaza picha hizo kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia simu ya mkononi aina ya Huawei ambazo zilikuwa zinamwonyesha Nuru Awadhi akifanya mapenzi.
Mshitakiwa alikana shtaka na hakimu Mjaya aliahirisha kesi hiyo hadi April 17,2017 itakapotajwa.
Social Plugin