Zipo sababu nyingi zimetajwa kuwa zinaweza kumfanya mtu aishi kwa furaha ambazo ni pamoja na kuamini katika kipato chako; kudumisha amani ya moyo huku ikitajwa furaha hiyo kuwa ni moja ya sababu zinazoweza kukufanya uwe na afya nzuri.
Leo nimekutana na hii ya njia sita ambazo furaha inaweza kuimarisha afya yako.
1: Furaha huulinda moyo wako
Utafiti unaonesha kuwa asili ya upendo na furaha siyo moyoni lakini husaidia kuulinda huku ikibainika kuwepo kwa uhusiano baina ya furaha na vipimo vingine vya afya ya moyo kama vile muda unaotumika wakati wa pigo moja la moyo na lingine na kuzilinganisha na hatari kadhaa za magonjwa ya moyo.
2: Furaha huimarisha mfumo wa kinga mwilini
Utafiti unaonesha kuwa mfumo wa kinga ya mwili hupanda na kushuka kutegemea na furaha aliyokuwa nayo mtu ambapo kuna uhusiano mkubwa baina ya furaha na mfumo imara wa kinga.
3: Furaha huzuia mkazo (stress)
Mkazo (stress) hausababishi matatizo ya kisaikolojia pekee bali pia husababisha mabadiliko ya ki-biology katika homoni zetu na shinikizo la damu. Furaha inatajwa kupoza hasira za athari hizi na wakati mwingine kutusaidia kurudi katika hali ya kawaida kwa haraka.
4: Watu wenye furaha hawaumwi mara kwa mara na huwa na kiwango kidogo cha maumivu
Watu ambao wana mood nzuri wana nafasi nzuri sana ya kuimarisha furaha ambayo huwasaidia kutoumwa homa za mara kwa mara na huwa na kiwango kidogo cha maumivu tofauti na watu ambao wana mood mbaya.
5: Furaha huzuia magonjwa na ulemavu
Furaha inatajwa kuhusika katika kuboresha hali ya makali ya homa za muda mrefu na mfupi na maumivu.
6: Furaha hurefusha maisha
Watu wenye furaha huweza kuishi kwa miaka 7-10 zaidi tofauti na wasiokuwa na furaha. Katika utafiti uliofanywa kwa wazee 4,000 wa Uingereza wenye umri wa miaka 52-79 ambao walikuwa na furaha mara nyingi zaidi kwa siku na kuonesha kuwa watu wenye furaha walikuwa chini ya 35% kufa ukilinganisha na watu ambao hawakuwa na furaha.
Social Plugin