Siku za hivi karibuni kumekuwa na mkanda wa video unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ambao anaonekana mwanamke mmoja akihojiwa akidai kuwa amezaa mtoto na Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima.
Katika video hiyo anaonekana mtangazaji wa Clouds Fm/Tv, Soudy Brown akimhoji mama huyo ambaye alisema kuwa amezaa mtoto na Askofu Gwajima. Mwanamke huyo anaeleza kuwa kazi yake yeye alikuwa akifanya usafi katika kanisa hilo kipindi likiwa Kawe kabla ya kuhamia Ubungo.
Hata hivyo, Clouds waligoma kuirusha hewani taarifa hiyo kwa madai kuwa haina mashiko, hali iliyomfanya mkuu wa Mkoa wa Dar Paul Makonda kuvamia ofisi hizo huku akiwa na Polisi
Kufuatia Tuhuma hizo, Leo Gwajima ametolea ufafanuzi suala hilo.
==>Tazama Video hapo chini
Social Plugin