Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAULI YA RIDHIWANI KIKWETE BAADA YA MAMA SALMA KIKWETE KUTEULIWA KUWA MBUNGE

Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani Ridhiwan Kikwete amefunguka baada ya mama yake jana kuteuliwa na Rais Magufili kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ridhiwan Kikwete amesema kuwa mama Salma Kikwete ni mwanamke wa shoka kwani amewezesha wasichana wengi nchini Tanzania kupata elimu na amekuwa mtetezi wa haki za wanawake hivyo anaamini kupata nafasi ya kuwa Mbunge itakwenda kuwezesha mapambano kuwa sheria rasmi.

"Umekuwa mtetezi wa haki za wanawake na usawa wa kijinsia, umewezesha wasichana kupata elimu. Wewe ni mwanamke wa Shoka. Hongera sana kwa uteuzi‬. Imani sasa umepata sehemu ya kuwezesha mapambano kuwa sheria. Mungu akutangulie Mama yangu , Mheshimiwa Mbunge. Hongera tena" aliandika Mhe. Ridhiwan Kikwete

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com