Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Kimenuka!! VYOMBO VYA HABARI TANZANIA VYAMTANGAZA RC MAKONDA KUWA ADUI...HAYA HAPA MAAMUZI MAZITO

Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds TV na kuwalazimisha watangazaji wa kipindi cha Shilawadu kurusha kipindi kinachomuhusu Askofu Gwajima kikiwa hakijamaliziwa maandalizi kinyume na taaluma ya habari, Leo Machi 22, 2017 Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limefanya kikao cha maamuzi dhidi suala hilo.

TEF pamoja na Club ya Waaandishi wa Habari Dar es saalam (DCPC) na Umoja wa Club za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) zimepitisha maamuzi matatu ikiwemo.

-Kulaani vikali vitendo vya RC Paul Makonda
-Kutoandika na kutangaza habari zozote kuhusu Paul -Makonda kwenye chombo chochote cha Habari.

-Kumtangaza RC Makonda kama adui wa Uhuru wa Vyombo vya Habari pamoja na yeyote atakayeshirikiana naye.

Unaweza kusoma kila kitu kwenye tamko hili hapa chini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com