Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KOMPYUTA YENYE SIRI YA KIKOSI CHA KUMLINDA RAIS YAIBIWA


Kompyuta ya kikosi cha kumlinda rais wa Marekani inayoripotiwa kuwa na michoro ya jumba la Trump Tower, na taarifa zingine za siri imeibwa kutoka kwa gari la afisa mmoja mjini New York.

Hata hivyo kikosi hicho cha kumlinda rais kinasema kuwa kompyuta hiyo huikuwa na taarifa za siri.

Lakini wanasema kuwa ina taarifa kuhusu uchunguzi wa aliyekuwa mgombea wa Democratic Hillary Clinton kutumia barua pepe ya kibinafsi.

Kwa sasa polisi wanachunguza kamera za siri kuweza kumtambua mshukiwa.

Shirika la ABC lilisema kwa gari la ajenti lililengwa katika eneo la Bath Beach kwenye mtaa wa Brooklyn.

CBS nayo ilisema kuwa kampyuta hiyo ilikuwa na taarifa muhimu kumhusu Papa Francis

Taarifa za polisi zililiambia gazeti la The York Daily News, kuwa taarifa zilizo kwenye kompyuta hiyo ni za siri kubwa.

Kompyuta hiyo inaripotiwa kuibwa kutoka kwa mkoba uliokuwa ndani ya gari. Mkoba huo hata hivyo umepatikana lakini kompyuta yenyewe bado inatafutwa.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com