Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiwa pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Salim Ahmed Salim mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com