Tulifanya mahojiano na wafanyakazi 14 wa kituo cha Clouds.-Balile
Tulifanya jitihada za kumtafuta Mkuu wa Mkoa, tulimpigia simu lakini hakupokea.- Balile
"Hata tulipofika katika ofisi yake, aliondoka kupitia mlango wa nyuma". -Balile
"Baada ya kushindwa kuonana naye, tukajiridhisha kuwa amechagua mwenyewe kutotumia fursa ya kuhojiwa". -Balile
'Imebainika ni kweli alikwenda pale Clouds na askari, waliingia kwenye vyumba ambavyo walipaswa kuingia kwa idhini maalumu'-Balile
"Kamati imejiridhisha pia kuwa palikuwa na vitisho kwa walinzi na wafanyakazi kwa kutumia askari wenye silaha". -Balile
"Miongoni mwa vitisho ni kuwalazimisha kurusha kipindi vinginevyo angewaingiza kwenye tuhuma za dawa za kulevya". Balile
'Makonda aliwatishia wafanyakazi Clouds kuwa angewafunga miezi 6 pia angewaingiza kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya'-Balile
Social Plugin