Viongozi wa dini pamoja na waumini wa Dini ya Kiristo jijini Dar es Salaam wametakiwa kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano katika kuwaukoa vijana katika vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya hapa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo katika Kanisa la KKKT usharika wa Kimara alipoungana na waumini wengine kwenye ibada ya maombi ya kumuombea Rais Dk. John Magufuli, Watendaji pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam dhidi ya mapambano dhidi ya maovu yakiwamo madawa ya kulevya.
Katika salamu zake RC Makonda amesema viongozi wa dini wanaweza kuibadilisha jamii ambayo inataka kupotea kupitia maneno ya Mungu, na kwamba watu wanaoingiza dawa za kulevya hawana nia njema na vijana ambao ndio nguvu kazi ya nchi hivyo wanahitaji kuokolewa katika lindi la matumizi ya dawa hizo ambayo ni janga kubwa katika taifa.
Aidha RC Makonda amesema kuwa ataendelea kusimama imara katika utekelezaji wa majukumu aliyopewa bila kuhofu wala kumuonea mtu yeyote.
Mchungaji Wilbroad Mastai (pichani) amesema waumini wana mchango mkubwa katika kuwasaidia viongozi kutokana na athari za dawa hizo na kutawaka kuondoa hofu kwa binadamu na kumtanguliza Mungu mbele.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiombewa na Askofu Mstaafu Mwamasika leo ibada ya maombi ya kumuombea Rais Dk. John Magufuli, Watendaji wa serikali pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam dhidi ya mapambano dhidi ya maovu ikiwemo dawa za kuevya jijini Dar es Salaam katika kanisa la KKKT Kimara jijini Dar es salaam leo.
Sehemu ya waumini katika katika Kanisa la KKKT Kimara jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na waumini wa Kanisa la KKKT Kimara ambalo leo limeendesha ya ibada ya maombi ya kumuombea Rais Dk. John Magufuli, Watendaji pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam dhidi ya mapambano dhidi ya maovu ikiwemo dawa za kulevya leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na waumini wa Kanisa la KKKT Kimara ambalo leo limeendesha ya ibada ya maombi ya kumuombea Rais Dk. John Magufuli, Watendaji pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam dhidi ya mapambano dhidi ya maovu ikiwemo dawa za kulevya leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Social Plugin