Mwanasheria Mkuu wa Chama na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana (ya polisi) iliyowekwa na wanasheria wawili, Hekima Mwasipu na Nashon Nkungu baada ya kushikiliwa na polisi kwa saa kadhaa jana.
Lissu alikamatwa ghafla alipokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya mashitaka yake ya uchochezo katika moja ya kesi zinazomkabili, kufutwa.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lissu alikamatwa na kushikiliwa kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi ambayo yangeweza kuibua mtafaruku wa kidini katika jamii wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Dimani, Zanzibar, mwezi Januari mwaka huu.
Baada ya mahojiano ya jana, Lissu ameachiwa kwa sharti la kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Machi 13, mwaka huu.
Social Plugin