Mgogoro wa Uongozi wa Chama cha Wananchi CUF umeendelea kufukuta ambapo Mwenyekiti wa Chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili Vyama vya Siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad baada ya Maalim Seif kukaidi wito wa Mwenyekiti wake kwenda Ofisi kuu Buguruni kwa zaidi ya mara nne
Prof. Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam pamoja na wafuasi wa chama hicho, amesema Maalim Seif amekaidi wito wa kwenda Makao Makuu Buguruni tangu Septemba 23 mwaka jana kwa ajili ya kusimamia mkutano wa kamati ya Utendaji ambao ulitakiwa kujadili mambo kadhaa ya chama hicho
Aidha, Prof. Lipumba amewavua madaraka wakurugenzi kutoka Zanzibar akiwemo Salim Bimani aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Omar Ali Salehe Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi, Abdalah Bakar Khamis Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Pavu Juma Abdallah - Haki za Binadamu, Mahima Ali Mahima Katibu Mtendaji JUVICUF pamoja na Yusuph Salim Naibu Mkurugenzi Ulinzi na Usalama CUF wote kutoka Zanzibar.
Chama cha Wananchi CUF kimekumbwa na Mgogoro wa uongozi tangu Prof. Lipumba alipotangaza kujiuzulu uongozi wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ambapo baadaye alitangaza kurudi na kufanyika mkutano mkuu ambao ulivurugika na kusababisha mpasuko kati ya CUF bara na CUF
Social Plugin