Msanii wa muziki wa asili nchini Mrisho Mpoto ameamua kumkingia kifua RC Makonda ambaye kwa siku za karibuni amekuwa aki-trend kwenye mitandao ya kijamii akituhumiwa kufoji vyeti.
Mpoto amedai anashangaa kuona hata wale ambao walikuwa wanamsupport na kumsifia mkuu huyo wameshinndwa kufungua midomo yao.
“Hii nchi ya ajabu sana ukifanya vizuri lazima upate maadui mpaka wakushushe, ndiyo waanze kumpansisha mwingine. Wako wapi waliosema Makonda songa mbele usirudi nyuma? mko wapi mliomuita Makonda shujaa mkombozi wa Wa watoto wetu, leo kila mtu anamruka na kuona hakuna alichofanya This is not Fair at all,”alianidika Mpoto Instagram.
“Angalieni utendaji wake Wa kazi na siyo vyeti vyake guys!! Songa Songa Songa Makonda kama ulivyosema hii vita siyo ndogo na ina wanafiki wengi. @paulmakonda @paulmakonda unawaona waleeeeeee ndiyo siyo watu wazuri kabisa!!,” aliongeza Mpoto.
Mkuu huyo hivi karibuni alidai hayo yote yamezalishwa kutokana na vita yake dhidi ya madawa ya kulevya ambayo umezaa matunda kwa kiasi kikubwa.
Social Plugin