Siku moja baada ya wekundu wa Msimbazi Simba kucheza mchezo wao wa 24 wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara dhidi ya Mbeya City na kulazimishwa sare ya 2-2, leo March 5 2017 ilikuwa zamu ya watani wao wa jadi Yanga kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Yanga ambao walikuwa na point 52 mchezo wao wa leo kama wangepata ushindi wangekuwa sawa kwa point na watani wao wa jadi Simba lakini Yanga wangepata nafasi ya kuongoza Ligi hiyo kwa kuwa na idadi kubwa ya magoli kuliko Simba.
Kutoka katika uwanja wa Jamhuri Morogoro Yanga wamelazimishwa sare tasa 0-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, licha ya kupata penati ambayo ilipigwa na Simon Msuva na kukosa penati hiyo, Simba sasa anaendelea kuongoza kwa tofauti ya point mbili dhidi ya Yanga ambao wana point 53.
Social Plugin